Chama Cha Mapinduzi

Kikao Kamati Kuu CCM: Wagombea Uwenyekiti wa wilaya za Moshi mjini, Hai, Siha, Makete Musoma Mjini na Vijijini wateuliwa

IKULU, DAR: Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimeanza rasmi kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.
 
58a43ba2-4f22-4fcb-a797-9b3cfc1b5349.jpeg
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017.
494e1321-2fa6-4f54-8c57-d47fb268e41b.jpeg
CCM kupitia Kamati kuu (CC) imefanya uteuzi wa wagombea walioomba kuwania nafasi ya Uenyekiti katika wilaya Sita nchini zikiwemo zile wilaya za kichama.
 
Wilaya ambazo zimepata wagombea ni Moshi Mjini, Siha na Hai zote za mkoani Kilimanjaro ambapo uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 1-2 mwaka huu. Wilaya ya Makete mkoani Njombe pamoja na wilaya zinazotambulika kichama za Musoma Mjini na Musoma Vijijini mkoani Mara uchaguzi wake umepangwa kufanyika Novemba 25-26 mwaka huu.
1.jpg
2.jpg

Add comment

Follow us

Don't be shy, get in touch. We love meeting interesting people and making new friends.